28 Machi 2025 - 02:26
Kiongozi wa Mapinduzi: Maandamano ya Mwaka huu yatakuwa miongoni mwa Maandamano yenye Heshima Kubwa katika Siku ya Quds

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Mwenyezi Mungu akipenda (Insha Allah), Matembezi (Maandamano) ya Mwaka huu yatakuwa miongoni mwa Matembezi bora zaidi, Matukufu na yenye Heshima Kubwa katika Siku ya Quds.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -; Ayatollah Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake wa Televisheni Usiku wa kuamkia leo (Ijumaa), alitathmini umuhimu wa Matembezi ya Siku ya Quds kwa mwaka huu kuwa ni zaidi ya miaka iliyopita na kusisitiza kuwa: Mwenyezi Mungu akipenda (Insha Allah), Matembezi ya mwaka huu yatakuwa miongoni mwa Matembezi bora zaidi, Matukufu na yenye Heshima Kubwa katika Siku ya Quds.

Nakala ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Maandamano ya Siku ya Quds daima ni ishara ya Umoja wa Taifa la Iran na Mamlaka ya Taifa la Iran; Vile vile ni ishara kwamba Taifa la Iran liko imara na endelevu katika malengo yake muhimu, ya kisiasa na ya kimsingi. Sio kwamba ni Taifa linatoa kauli mbiu ya kuunga mkono Palestina, kisha liachane na kuunga mkono Palestina baada ya mwaka mmoja au miwili. Kwa muda wa miaka arobaini (40) na isiyo ya kawaida Taifa la Iran limekuwa likishiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, katika hali ya hewa ya baridi, na hali ya hewa ya joto, kwa midomo iliyofunga saumu, kote nchini, na si maeneo ya Mijini tu; bali ni katika Miji mikubwa, Miji midogo na hata Vijijini. Kwa hivyo, Maandamano ya Siku ya Quds ni moja ya fahari za Taifa la Iran.

Mwaka huu, kwa maoni yangu, Maandamano haya ni muhimu zaidi. Mataifa ya dunia nzima yanatuunga mkono; Wale wanaotujua wanapendelea Taifa la Iran, lakini baadhi ya sera na Serikali zinazopingana na Taifa la Iran zinaeneza propaganda za chuki dhidi ya Taifa la Iran kwamba: Wanataka kujifanya wanaonyesha kuwa kuna tofauti na ikhtilafu; Wanajifanya kuonyesha kuwa kuna udhaifu. Maandamano yenu katika Siku ya Quds yatakataa hila zote hizi na kuyabatilisha maneno hayo ya batili.

Natumai, Mwenyezi Mungu akipenda (Insha Allah), atakuwafikisheni na kukusaidieni katika Matembezi ya Siku ya Quds kuwa mojawapo ya Matembezi bora zaidi, na Matukufu zaidi, na yenye heshima zaidi katika miaka hii michache.

Amani iwe juu yenu, na baraka za Mwenyezi Mungu pia ziwe juu yenu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha